HUYU HAPA MRITHI WA PLUIJIM SINGIDA UNITED
TIMU ya Singida United imemthibitisha Mrundi, Etienne Nayiragijje kuwa kocha wake mpya, akichukua nafasi ya Mholanzi, Hans van der Pluijm anayeondoka.
Pluijm anaondoka Singida United baada ya msimu mmoja na taarifa zinasema Mholanzi huyo anahamia Azam FC ambao wanajipanga upya baada ya msimu huu mbaya kwao chini ya Mromania, Aristica Cioaba ambaye tayari amekwshaondoka.
Bin Zubeiry Sports - Online inafahamu kwamba Ndayiragijje ambaye amekwishaachana na Mbao FC aliyoiongoza kwa misimu miwili akitokea kwao Burundi.
Msimu uliopita, Ndayiragijje pamoja na kunusurika kuishusha Mbao FC, lakini aliiwezesha kufika fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) ambako ilifungwa na Simba SC 2-1 Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Na msimu huu, Ndayiragijje aliingia kwenye mtafaruku na uongozi wa klabu hiyo ya Mwanza baada ya mzunguko wa kwanza tu wa Ligi Kuu na kuondoka, nafasi yake ikichukuliwa na mchezaji wa zamani wa Pamba SC, Fulgence Novatus.
Pluijm yeye aliichukua Singida United baada ya kupanda Ligi Kuu, kufuatia kufukuzwa Yanga SC na amefanikiwa kuifikisha fainali ya ASFC ambako itamenyana na Mtibwa Sugar Juni 2, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.