VPL OKWI KUIVUNJA REKODI YA JERSON TEGETE LEO?

Na Joseph michael
Katika wachezaji wote waliowahi kupita Simba na Yanga na kufunga mabao Aprili katika mechi ya watani wa jadi ni Emmanuel Okwi pekee anayeweza kuivunja rekodi ya Jerry Tegete ya kufunga mabao matatu.

Wachezaji wengi wameshaondoka wengine wakiwa wameshastaafu soka, lakini Okwi bado ni mshambuliaji tegemeo katika kikosi cha Simba na leo atakiongoza kikosi chake kuivaa Yanga.

Okwi aliisaidia Simba kuifunga Yanga bao 1-0 Aprili 18, 2015 hivyo kama atafunga mabao mawili kesho ataifikia rekodi Tegete aliyoweka miaka nane iliyopita.

Tegete anayechezea Majimaji ya Songea kwa sasa alifunga bao lake la kwanza Aprili 19, 2009, Yanga ilipolazimishwa sare mabao 2-2 bao lingine lilifungwa na Ben Mwalala huku mabao ya Simba yakifungwa na Haruna moshi Boban na Ramadhan Chombo'Redondo' ambao hivi sasa wanaichezea Friends Rangers.

Pia, Tegete alifunga mabao mawili Aprili 18, 2010, Yanga ilipopokea kipigo cha mabao 4-3 kutoka kwa Simba. Bao lingine la Yanga lilifungwa na Athuman Iddi 'Chuji' wakati mabao ya Simba yalifungwa na Mussa Hassan Mgosi aliyefunga mawili ,Uhuru Seleman na Hilary Echesa.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.