Yanga Wamtaka Lwandamina Kwenda Ethiopia..
Uongozi wa Yanga umekiri kupokea barua ya kujiuzulu kwa kocha wake Mkuu George Lwandamina anayedaiwa kusaini mkataba wa awali kuitumikia ZESCO FC ya Zambia.
Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema uongozi umepokea barua yake ya kujiuzulu na tayari wameijibu barua hiyo.
Mkwasa amesema wamemuagiza kocha huyo kujiunga na kikosi cha Yanga nchini Ethiopia kwa ajili ya mchezo wa marudiano kombe la shirikisho dhidi ya Wolaitta Dicha.
Licha ya Mkataba wake kuelekea ukingoni, Mkwasa amesema Yanga ilikuwa bado na malengo nae wamemtaka kuhakikisha anamaliza muda wake wa mkataba uliobaki.
Aidha Mkwasa ameongeza kuwa kwa sasa Yanga itakuwa chini ya Kocha Mkuu Noel Mwandila na atasaidiwa na Shedrack Nsajigwa.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.