Yanga Kurejea Dar Leo
Kikosi cha Yanga kinarejea jijini Dar es salaam leo kutoka mkoani Morogoro tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Simba utakaopigwa keshokutwa Jumapili, April 29 2018.
Mchezo huo utapigwa kwenye uwanja wa Taifa.
Yanga iliweka kambi ya siku tano mkoani Morogoro kujiandaa na mchezo huo.
Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema maandalizi ya kuelekea mchezo huo yamekamilika na amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa kuiunga mkono timu ili iweze kuibuka na ushindi.
Ten amesema tiketi zinapatikana Makao Makuu ya klabu ya Yanga.
Msemaji huyo wa Yanga ameongeza kuwa wachezaji wote waliokuwa kambini mkoani Morogoro wako tayari kwa mchezo huo isipokuwa mshambuliaji Donald Ngoma ambaye bado ni majeruhi.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.