SIMBA YAWATAKA MASHABIKI KUJITOKEZA KWA WINGI JUMAPILI
Klabu ya Simba imewataka mashabiki wake kujitokeza kwa wingi katika mchezo wa ligi dhidi ya watani wao wa jadi Yanga siku ya Jumapili ili kuwapa sapoti wachezaji wao.
Mchezo huo wa mzunguko wa pili wa ligi utafanyika katika uwanja wa Taifa huku Wekundu hao wakiwa juu kwa tofauti ya pointi 11.
Msemaji wa klabu ya Simba, Hajji Manara amewataka mashabiki hao kununua tiketi kwa mawakala wa Selcom ili kuhakikisha wanahudhuria kwa wingi.
Manara amewaasa kuacha kununua tiketi kwa watu binafsi kwakua wanaweza kuuziwa feki na wakashindwa kuingia uwanjani hali ambayo itasababisha vurugu.
"Niwaombe mashabiki wetu kuja kwa wingi uwanjani Jumapili kutoa sapoti kwa wachezaji ili tupate ushindi, tena wahahakishe wananua tiketi kwa mawakala wa Selcom kwa ajili ya kuondoa usumbufu," alisema Manara.
Wakati huo huo Manara amewaasa mashabiki watakaojitokeza uwanjani kujizuia na jazba hata kama watakuwa hawajatendewa haki na mwamuzi ili kudumisha amani.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.