Yanga Dimbani Leo Bila Lwandamina Na Wengine Watatu
Klabu ya Yanga leo Jumatano ya April 11 itashuka katika dimba la Taifa Dar kucheza mchezo wa raundi ya 22 ya vpl dhidi ya Singida United majira ya saa kumi jioni.
Kuelekea mchezo huo klabu ya Yanga itawakosa wachezaji wake watatu Amis Tambwe ambaye ni majeruhi wa muda mrefu, Donald Ngoma aliyejitonesha majeraha kwenye mazoezi ya timu hiyo ikijiandaa na Waleyta dicha, na Andrew Vincent Dante ambaye alipata majeruhi kwenye mchezo wa mtoano wa Caf Confederation Cup dhidi ya Waleyta Dicha ya Ethiopia
Pia klabu hiyo imepata pigo kubwa baada ya taarifa ya kocha wao mkuu George Lwandamina kujiunga na mabingwa wa Zambia, Zesco United hapo jana na leo hatakuwa sehemu ya mchezo huo.
Viongozi wa klabu hiyo wamesema watalitolea ufafanuzi wa kina suala la Lwandamina kutangazwa kuwa kocha wa Zesco United.
Mpaka sasa Klabu ya Yanga imecheza mechi 21 za Vpl ina pointi 46 katika nafasi ya 2 kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara huku Singida wakiwa nafasi ya 5 wakiwa na pointi 36 baada ya kucheza michezo 23.
Yanga na Singida wamekutana katika mechi 4 (1 Kirafiki, 1 vpl, 1 Mapinduzi Cup na 1 Asfc) huku Yanga akishinda mechi 1 wa kirafiki, Singida naye ameshinda mechi 1 wa Asfc kwa penati na wametoa sare katika michezo 2 (vpl na Mapinduzi Cup)
@yossima Sitta Jr.
Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.