TETESI: Wachezaji wa Tanzania wazamia Australia
Baada ya mashindano ya Jumuia ya Madola kumalizika huko nchini Australiakwenye mji wa Gold Coast siku ya Jumapili ambapo Tanzania ilipeleka wanamichezo 16 kushiriki katika michezo mbalimbali, inaelezwa kuwa baadhi ya wanamichezo wametoroka kambini na kuelekea kusikojulikana.
Mmoja alikuwa akishiriki mpira wa meza huku mwingine akiwa ni bondia, taarifa hizo zimekanushwa na Baraza la Michezo Tanzania (BMT) kupitia kwa msemaji wake Najaha.
“Hatuna taarifa rasmi ambayo tumeipata kuhusiana na ambao wameenda kwenye mashindano ya madola na wameingia mitini kwa sababu kuna mkuu wa msafara ambaye ni mkurugenzi michezo ambaye ndiye alienda na timu ya wachezaji kwenye mashindano ya Jumuia ya Madola.”
“Kwa hiyo watakaporudi rasmi nadhani taarifa hiyo itatolewa na serikali na tutaju ni kipi kilichotokea kwamba wako wapi na wako wapi lakini kwa sasa hatuna taarifa rasmi.”
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.