Sakata La Ngoma Laibuka Upya Yanga


Kuondoka kwa kocha George Lwandamina huenda kukaliibua sakata la mshambuliaji Donald Ngoma ambaye ameichezea Yanga michezo mitatu tu msimu huu.

Lwandamina aliyetimkia ZESCO, ameeleza kuwa moja ya sababu zilizomfanya 'ajiweke' pembeni akisubiri mkataba wake umalizike ni pamoja na sintofahamu inayomuhusu mchezaji huyo.

Lwandamina ameushushia lawama uongozi wa Yanga chini ya Katibu Mkuu Charles Mkwasa kwa 'kumlea' mchezaji huyo ambaye sababu zake za kutorejea dimbani haziridhishi.

Amesema amelalamika uwepo wa Ngoma kikosini unachangia kushusha morali ya wachezaji wengine sababu wanaona kama anapendelewa.

Ngoma ndiye mchezaji anayelipwa mshahara mnono zaidi ndani ya kikosi cha Yanga licha ya kuwa ndiye mchezaji aliyecheza michezo michache zaidi kikosini.

Licha ya kutolipwa mishahara kwa miezi mitatu, Lwandamina amesema hilo silo tatizo lililomuondoa Yanga wakati huu, bali kutozingatiwa kwa mapendekezo yake mbalimbali aliyoyatoa kwa uongozi ikiwemo mambo ya maslahi ya wachezaji.

Uongozi wa Yanga umeitisha Mkutano na waandishi wa habari leo na huenda ukweli wa sakata hilo la kocha George Lwandamina ukawekwa wazi.

Kwa mashabiki na wanachama wa Yanga, ni vyema kusubiri maelezo ya upande wa uongozi kabla ya kuwahukumu baadhi yao waliotuhumiwa na kocha George Lwandamina.

Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.