Ndemla Kumpoteza Tshishimbi
KIUNGO wa Simba, Said Ndemla wala hana maneno mengi kuhusu mchezo wa Jumapili dhidi ya Yanga lakini alichowaambia mashabiki wa timu yake ni kwamba waje pale Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kushuhudia burudani.
Akimzungumzia kiungo wa Yanga Papy Tshishimbi ambaye kama atapata nafasi ya kuanza atakutana nae katika dimba la kati, alisema mchezaji huyo ni mzuri lakini atajitahidi kufanya vizuri katika mchezo huo ili kumfunika.
“Uwezo wake haujifichi ni mchezaji mzuri, lakini naamini kikubwa tukiwa vizuri katika nafasi hiyo tutaweza kumdhibiti asilete madhara kwetu,” alisema.
Ndemla ambaye anacheza Ligi Kuu kwa mwaka wa nne sasa, aliliambia gazeti la Mwanaspoti kwamba mchezo huo ni mgumu na hautabiriki kutokana na timu zote kufanya maandalizi kwa utulivu.
“Ni ngumu kusema kwamba nani atakuwa mshindi au kama tukishinda hapa ndio atakuwa bingwa, dakika 90 za uwanjani ndio zitaamua kwamba nani ni bora zaidi ya mwenzake,” alisema.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.