Mbeya City Na Singida United Hakuna Mbabe.


Timu za Mbeya City na Singida United zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya bao moja katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Mlinzi Haruna Shamte aliwapitia wenyeji bao la kwanza dakika ya tano kwa mpira wa adhabu uliotinga moja kwa moja wavuni nje ya 18.

Singida walisawazisha bao hilo dakika ya 16 kupitia kwa mlinzi Malik Antiri kwa kichwa baada ya mpira wa adhabu uliopigwa na Shafiq Batambuze.

Singida imeshindwa kupata matokeo ya ushindi kwenye michezo ya ligi katika siku za karibuni ikiambulia sare.

Mchezo huo ulikuwa wa kasi kwa pande zote kushambuliana kwa zamu lakini safu zote za ushambuliaji  zilikosa umakini.

City imefikisha pointi 28 ikiwa nafasi ya tisa kwenye msimamo wa ligi huku Singinda ikiwa ya tano na alama 38

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.