Mtibwa Yatangulia ASFC Baada Ya Kuiondoa Stand United.
Mtibwa itakutana na mshindi kati ya Singida United na JKT Tanzania katika mchezo wa fainali utakaofanyika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha Juni 2.
Stand walionekana kushindwa kuhimili vishindo vya Wakata miwa hao mapema baada ya kufanya makosa mengi dakika za mwanzoni.
Kiungo Hassan Dilunga alipeleka kilio kwa Wapiga debe hao baada ya kufunga mabao yote mawili dakika za 30 na 39.
Vijana wa kocha Zuberi walistahili kuingia hatua hiyo kutokana na uwezo mkubwa waliuonyesha.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.