Lipuli: "Tutasameheana Sana Na Mbao, Hatutakuwa Na 'semile'."


Kikosi cha wachezaji 23 kimewasili salama jijini Mwanza jana majira ya saa moja usiku kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbao Fc.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa msemaji wa klabu hiyo inaleza kuwa wachezaji wako vizuri na hakuna majeruhi  mpaka sasa.

Kwa uchache  tu kikosi kiko imara, hatuna majeruhi hata mmoja, wachezaji wana morali iko juu.

Aidha ameongeza kwa kusema kuwa katika mchezo huo wanatambua umuhimu wake na pointi tatu ni muhimu na Mbao watawasamahe kwa kile kitakachotokea.

Tumejiandaa vya kutosha ,tunauhakika wa kupata ushindi mkubwa katika mchezo wetu huo, tunahitaji sana alama tatu, tutasameheana sana na wenzetu Mbao, hatutokuwa na 'semile'.

Asubuhi hii kikosi kimefanya mazoezi uwanja wa CCM kirumba ikiwa ni siku moja kabla mchezo

Mchezo huo utapigwa kesho kwenye dimba la CCM Kirumba.


Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.