Kinachomuumiza Tambwe Yanga
Mshambuliaji wa Yanga Amissi Tambwe amewapongeza wachezaji wenzake kwa kufanikiwa kutinga hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Tambwe amesema alitamani kuwa sehemu ya kikosi hicho kilichoandika historia nchini Ethiopia lakini majeraha yamemnyima fursa hiyo.
Aidha Tambwe ameeleza kufarijiwa na uungwaji mkono anaopewa katika kipindi hiki kigumu.
"Nawapongeza wachezaji wenzangu kwa kufanikiwa kuingia kwenye hatua ya makundi, Nawashukuru wanayanga kwa jinsi wanavyonisapoti wakati huu wa majeraha yangu,naumia sana kutokucheza lakini hili ndiyo soka, " Tambwe ameiambia Yanga TV.
Jana Yanga ilifanikiwa kutinga makundi kwa kuiondoa Wolaitta Dicha ya Ethiopia kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1.
Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuwasili leo kuamkia kesho usiku saa saba na dakika 10.
Leo mchezaji wachezaji wa Yanga walialikwa nyumbani kwa Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.