Hans: Bao la Yanga ni la offside


Kocha mkuu wa timu ya soka ya Singida United Mholanzi Hans Van Der Pluijm ameonesha kuhuzunishwa na bao la kusawazisha la Dar Young Africans lililofungwa na mlinzi Abdallah Shaibu akidai kuwa kuna mchezaji mmoja wa Yanga alitaka kuucheza mpira kabla ya bao kufungwa alikuwa offiside.

Hans amesema anashindwa kuelewa kwanini Mwamuzi msaidizi namba moja Ferdinand Chacha hakumuona Yusuph Mhilu ambaye alikuwa offside na alijaribu kuucheza mpira kabla ya Shaibu kufunga akiwa pekee yake.

"Kwa maoni yangu ilikuwa ni offiside goal kwa sababu mchezaji mmoja wa Yanga (Yusuph Mhilu) alikuwa kwenye mstari wa kuotea na kutaka kuugusa mpira, niseme alikuwa tayari ameotea na jambo ambalo liliwachanga mabeki wangu kabla ya Shaibu kufunga, nadhani hili linawasumbua sana marefarii," amesema Hans.

Sare ya 1-1

Katika mchezo huo Singida United walilazimishwa sare ya bao 1-1 na mabingwa watetezi Dar Young Africans, kwani wao ndio walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 3 kupitia kwa Papy Kambale kabla ya Yanga kusawazisha katika dakika ya 45 ya mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam

Matokeo hayo yanawafanya Singida United kufikisha alama 37 na kuendelea kukalia nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi, wakati Yanga wao wanakuwa wamefikisha alama 47 katika nafasi ya pili, nafasi tano nyuma ya vinara Simba SC.


Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.