Chirwa Aondoka Nchini..
Uongozi wa Yanga umemruhusu mshambuliaji wake Obrey Chirwa kwenda kwao nchini Zambia kushughulikia matatizo ya kifamilia imefahamika.
Chirwa hatakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kitakachoivaa Welayta Dicha keshokutwa Jumamosi kwenye mchezo wa kwanza wa kusaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho.
Mshambuliaji huyo kinara wa mabao kwenye kikosi cha Yanga anatumikia adhabu ya kadi mbili za njano katika michuano ya CAF sambamba na Papi Tshishimbi, Kelvin Yondani na Said Juma Makapu.
Meneja wa Yanga Hafidh Saleh amesema Chirwa aliomba ruhusa uongozi wa klabu hiyo na wamemruhusu.
Yanga iko mkoani Morogoro kujiandaa na mchezo dhidi ya Welayta Dicha na inatarajiwa kurejea jijini Dar es salaam leo.
Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.