Bocco: Itakuwa Ni Aibu Kubwaa.
Mshambuliaji wa Simba, John Bocco amesema itakuwa ni aibu kubwa endapo klabu yake ya Simba itashindwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara msimu huu.
Akiongea na mtabdao wa goal.com bocco amesema kuwa wanayo nafasi ya kutwaa ubingwa na kuwahmfanya mashabiki wao kuwa na furaha.
Tunatakiwa kuwafanya mashabiki wetu wawe na furaha, tutapambana mpaka mwisho kuhakikisha tunatwaa ubingwa , itakuwa ni aibu kama hatutatwaa ubingwa.
Simba kwa sasa ipo kileleni mwa ligi hiyo ikiwa pointi 11 mbele ya mabingwa watetezi wa ligi hiyo Yanga ambao wapo katika nafasi ya pili na pointi 47 huku wakiwa na michezo miwili mkononi.
Simba kama itafanikiwa kutwaa ubingwa huo basi itakuwa ni mara ya pili kwa Bocco kutwaa ubingwa huo baada ya ule aliouchuku akiwa na Azam FC 2013.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.