Bayern Munich Wamtaja Mrithi Wa Jupp Heynckes


Bayern Munich wamemtangaza kocha wa Eintracht Frankfurt, Nico Kovac kuwa kama kocha mpya wa Bayern pale Jupp  Heynckes atakapoondoka mwishoni mwa msimu huu.

Inaonekana kama The Bavarians walikuwa wanamtaka kweli kwani imewalazimu kuilipa Frankfurt "Release Clause" ya paundi millioni 1.9 ili kupata huduma za mwalimu huyo, na "Release Clause" hiyo ilikuwa ni endapo tu Bayern watamtaka au klabu mbili za nje.

Nico Kovac 46, alikuwa na mkataba na Frankfurt mpaka 2019, Bayern wamempa kandarasi ya miaka 3 ikiwa haijawekwa wazi atalipwa mshahara kiasi gani.

Jupp aliweka wazi hatoendelea zaidi ya msimu huu akija kuchukua nafasi ya Ancelloti mwezi wa 10 mwaka jana ambaye alitimuliwa, Kovac anaanza kazi rasmi Julai 1 mwaka huu.

Taarifa hii imekuja kama ya kushangaza kwani hakukuwa hata na tetesi zake na pia mashabiki wameonekana kutopendezewa na taarifa hii kwani wanaona Kovac bado hajafikia mafanikio mengi kama kocha na pia hana uzoefu wa mashindano ya ulaya na kujiuliza kama kweli ataweza kuendana na presha ya kufanya kazi kwenye klabu kubwa kama Bayern Munich, tukumbuke hayo hayo yalisemwa kwa Guardiola akipewa mikoba ya Barca.


Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.