BANDA ATUPIA MBILI BAROKA IKITOKA SARE DHIDI YA CELTIC AFRIKA KUSINI
Na Joseph michael
Mchezaji wa kimataifa kutoka Tanzania, Abdi Banda, ameibuka shujaa kwenye mchezo wa leo baada ya kuifungia timu yake mabao mawili ikiwa nyumbani na kufanya mchezo huo uende sare ya 2-2 dhidi ya Bloem Celtic.
Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini, Banda alipasia kambani mabao hayo katika dakika za 61 na 69, huku wapinzani wakifunga kupitia kwa Sepana Letsoalo mnamo dakika ya 59 na Lucky Baloyi kwenye dakika ya 85.
Matokeo hayo yameifanya Baroka ipande mpaka nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi huku ikijikusanyia jumla ya pointi 34 ikicheza michezo 29

No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.