AZAM KUINGIA KAMBINI LEO KUJIWINDA NA MTIBWA


Kikosi cha timu ya Azam FC kinatarajiwa kuingia kambini leo kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa Manungu Aprili 28.

Azam imeshindwa kufanya vizuri katika michezo mitatu ya ligi iliyopita ambapo ilipoteza mchezo moja na kutoka sare mbili.

Msemaji wa klabu hiyo, Jaffer Idd amesema kuwa wameamua kuingia kambini mapema kwakua wanafahamu utakuwa mchezo mgumu kutokana na uimara wa Mtibwa.

"Aprili 28 sio mbali tunaingia kambini kesho kujiandaa na mchezo dhidi ya Mtibwa ambao tutacheza Manungu, matokeo yetu ya karibuni sio mazuri sana," alisema Jaffer.

Azam ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 46 baada ya kucheza michezo 25.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.