Watatu Yanga Kuukosa Mchezo Wa Kwanza wa Confederation Cup Sababu Hii Hapa, Ngoma Kuziba Nafasi Mojawapo
Klabu ya Yanga itawakosa wachezaji wake muhimu Papi Tshishimbi, Obrey Chirwa na Said Juma 'Makapu' kwenye mchezo wa kwanza wa mtoano wa kombe la Shirikisho dhidi ya Wolaitta Dicha fc ya Ethiopia utakaopigwa kati ya April 06-08.
Wachezaji hao wote wamefikisha kadi mbili za njano baada ya kupata kadi kwenye mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers Jumamosi iliyopita.
Kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo yanayosimamiwa na CAF, wanapaswa kukosa mchezo mmoja.
Adhabu kama hiyo ilimkumba beki Hassani Kessy ambaye alikosa mchezo dhidi ya Township Rollers.
Hata hivyo kurejea kwa Donald Ngoma kikosini kumeipa ahueni Yanga kuelekea mchezo huo wa kwanza utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Aidha kukosekana kwa Tshishimbi na Makapu kwenye mchezo huo kutawapa nafasi chipukizi Maka Edward na Pato Ngonyani kurejea kwenye kikosi cha kwanza.
Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.