UTEUZI WA NYAMLANI NA KUBADILI KAMATI YA RUFAA NI UCHAKACHUAJI UNAIVUNJA KATIBA
-Makamu wa rais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania ambaye amekata rufaa kupinga adhabu ya kufungiwa bila kufuata sheria. Amelaani ukiukwaji wa katiba unaofanywa na TFF na kuitaka Serikali iingilie kati kukomesha mchezo mchafu.
-Kamati tendaji ya TFF imemteua Athuman Nyamlani kuwa kaimu makamu wa Rais ni kinyume na ibara ya 34 ya katiba ya TFF ambayo haitoi mamlaka ya uteuzi kwa kamati tendaji kwa uteuzi wa Bw. Nyamlani, TFF imevunja ibara ya 34(1) a-q ya Katiba ya TFF toleo la mwaka 2015
-Kamati ya Tendaji pia imebadili wajumbe wa kamati ya maadili ya rufaa ya TFF na kuwaweka watu wapya wakati tayari Michael Wambura amekata rufaa kwa mabadiliko hayo TFF imevunja Ibara ya 34(2) ya Katiba ya TFF inayosema
"Judicial organs and election Committees are independent and their members shall not be removed before the end of their tenure without endorsement of the General Assembly"
-Maana yake ni kwamba vyombo vya kutoa haki vya TFF ni huru na wajumbe wake hawataondoka kabla au kumaliza muda wao bila idhini ya mkutano mkuu.
-Bwana Michael Wambura anatafasiri ukiukwaji huu wa maksudi wa katiba kama mchezo mchafu unaolenga kumdidimiza katika kudai haki yake.
-Wambura alifungiwa bila kusikilizwa na kamati isiyo na mamlaka na baada ya kukata rufaa kwa hati ya dharura, Rufaa yake imecheleweshwa kwa maksudi wakati wajumbe wote wapo Dar isipokuwa mmoja tu.
-Walifanya hivyo ili kwanza waiitishe mkutano wa kamati tendaji kumteua Nyamlani na pili wabadilishe wajumbe wa kamati ya rufaa itakayosikiliza rufaa ya Wambura na kuweka watu ambao wana uhakika kuwa watafuata maelekezo yao
-Bwana Wambura ameiomba serikali iingilie kati mara moja kuzuia ukiukwaji wa katiba na Sheria na iwaelekeze TFF waitishe kikao cha kamati ya Rufaa bila mabadiliko yoyote ili haki itendeke kwake.
Amendika Emmanuel Muga
Wakili wa Michael Wambura
@yossima Sitta Jr.
Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.