Ukiachilia Mbali Danny Usengimana, Huyu Hapa Mchezaji Mwingine Anayataka Kuachana Na Singida United
Siku chache zilizopita nyota wa klabu ya Singida United na raia wa Rwanda, Danny Usengimana wa Singida United ameamua kuachana na klabu hiyo kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni kutokufuatwa kwa makubaliano waliyowekeana, kwa sasa kuna taarifa zinazoendelea kwa chibi zikidaiwa kuwa nyita mwingine, Rusheshangoga Michel naye yupo mbioni kuondoka kunako klabu hiyo kutokana na muda kuendelea kupita bila kulipwa maslahi yake ya Usajili.
Danny Usengimana aliwasili nchini Rwanda machi 27.2018 na kutangaza kuwa amerejea kutokana na kutofikia maafikiano waliyokubaliana licha ya uongozi kufahamu kama kareje.
Aidha kwa muujibu wa chanzo cha kuaminika kimeeleza kuwa Rusheshangoga naye anaweza kuondoka endapo atakuwa hajalipwa maslahi yake bila hata kumaliza ligi ambayo kwa sasa imesaliwa na michezo 8 pekee.
Aidha kwa muujibu wa chanzo cha kuaminika kimeeleza kuwa Rusheshangoga naye anaweza kuondoka endapo atakuwa hajalipwa maslahi yake bila hata kumaliza ligi ambayo kwa sasa imesaliwa na michezo 8 pekee.
Ikumbukwe kuwa Danny na Rusheshangoga walijiunga na Singida United msimu wa 2017/18 kwa mkataba wa kuitumikia klabu hiyo kwa miaka miwili.
Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.