Mambo Ni Hivi Azam Sports Fedaration Cup Leo


Mpaka kesho jioni timu nne zitakazokuwa zimetinga nusu fainali ya kombe la FA zitakuwa zimefahamika baada ya michezo yote ya robo fainali kukamilika.

Jana Stand United ilikuwa ya kwanza kutinga hatua hiyo baada ya kuilaza Njombe Mji kwa bao 1-0.

Leo Azam FC itaikaribisha Mtibwa Sugar katika mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Mchezo mwingine utapigwa mkoani Mbeya ambapo maafande wa Tanzania Prisons watakuwa wenyeji wa Polisi Tanzania.

Kesho Jumapili Singida United na Yanga zitahimisha mchezo wa nne wa robo fainali zitakapo pepetana kwenye uwanja wa Namfua.

Bingwa wa michuano hiyo itajinyakulia kitita cha Tsh Mil 50 pamoja na kuiwakilisha Tanzania Bara kwenye michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika mwakani.

Bingwa wa msimu uliopita Simba, ilitolewa katika hatua za awali kabisa na timu ya Green Worriors inayoshiriki ligi daraja la Pili

Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.