TUAMKE USINGIZINI KAMA TAIFA KISOKA


Vilabu vya wenzetu nje vinafanikiwa kwa mambo mengi sana lakini kubwa katika hayo ni ubora wa wachezaji wa ndani ambao kwa sehemu kubwa ndio wanasajiliwa kwenye vilabu hivyo.

Ubora wa wachezaji wa ndani unatokana na mambo mengi sana;

1. Misingi bora ya soka la vijana
2. Sera nzuri kitaifa kusimamia ukuaji na uendelezwaji wa mchezo husika
3. Viongozi bora katika soka wenye weledi stahiki kuendesha vilabu , vyama , Shirikisho na mabaraza ya michezo
4. Uchumi bora

Yapo mengi kuyataja lakini tukianzia hapo itakuwa sawa .

Ukiwa na quality players kwenye ligi zote ni dhahiri bingwa atatokana na ubora wake kimbinu na kiufundi nakusimama vyema ndani na nje ya mipaka.

Mathalani ligi kuu inayobeba takribani wachezaji 400+ ikiwa na wachezaji wazawa walioandaliwa vyema na vipaji sahihi chini ya utawala bora ni lazima kiwango cha ligi kiwe bora kitakachopelekea kuwa na timu za taifa nzuri na vilabu vinavyotoka nje kuwa bora.

Hatuna uwezo wa kusajili wachezaji wenye viwango bora kutusaidia kimataifa hivyo ni lazima tuvigeukie viwango vya wachezaji wa ndani.

Endapo vilabu vyetu vikiwa na wacheza wazawa wenye viwango vizuri walioandaliwa vyema kwenye misingi bora ni dhahiri watatoa mchango mzuri kimataifa wanapochanganyikana na wachezaji toka nje wenye viwango bora zaidi .

Ukiwa na lundo la averaged players wazawa hata ukiwa na wachezaji bora toka nje ni ngumu kupata matokeo chanya kwa sababu wingi wao una impact kwa wageni pia ni ngumu kwao kujifunza au kuziba pengo wanapoumia matured players from outside.

Tujitathimini kama taifa katika viwango vya wazawa ili tuweze kuimarika kimataifa.

Viwanda vingi nchini vilikufa baada ya sera ya soko huria , ubinafsishaji na kuruhusu uwekezaji toka nje pasi kupima madhara ya bidhaa na viwanda vya ndani katika mzingo huo wa ‘ soko huria ‘ . Hii ni sawa kabisa na kiwanda chetu cha soka . Tulipoua UMITASHUMTA na UMISETA tulivimaliza viwanda mama vya kuzalisha wachezaji wetu kushindana na mfumko wa katikati ya miaka ya 90 mpaka sasa wa ujio wa wachezaji wa kulipwa toka nje.

Bila kurudi kwenye misingi bora kisoka tutaendelea kusindikiza wenzetu kwa maneno dhaifu ya kujifariji kufa kiume au kishujaa.

@ Samuel Samuel
2018

Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.