Tanzania yaporomoka nafasi 16, viwango vya soka Ulimwengu


Soka la Tanzania kwa upande wa wanawake limeshuka kwa nafasi 16 katika viwango vya ubora wa soka ulimwengu vinavyotolewa na Shirikisho la Soka Ulimwengu (FIFA).

Tanzania ambayo katika viwango vilivyopita ilikuwa ikishika nafasi ya 102, imeshuka na kutopewa nafasi yoyote kutokana na kutocheza mchezo wowote kwa miezi 18, ikiwa na alama 960 ambazo ni alama sawa na zile walizopata mwezi Disemba mwaka jana.

Viwango hivyo vimetolewa wakati ambapo timu ya Taifa ya wanawake inajiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwenye fainali za Mataifa Afrika dhidi ya Zambia April 4 mwaka huu.

Wapinzani wa Twiga Stars, Zambia (She-Polopolo) wapo nafasi ya 98 duniani.

CECAFA

Kwa upande wa timu za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) Kenya imeshika usukani ikiwa nafasi ya 108, ikifutiwa na Ethiopia, Tanzania, Eritrea, Rwanda, Uganda na Burundi.

Kwa upande wa Duniani Marekani wameendelea kuongoza wakifuatiwa na England katika nafasi ya pili na nafasi ya tatu ikishikwa na Ujerumani.

Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.