Sio Siri Tena , Anatua Yanga..


Ule usemi usemao kwamba "Ukiona manyoya basi ujue kashaliwa" huenda ukajidhihilisha wazi katika hili.

Kumekuwa na taarifa mbalimbali ambazo zimekuwa zikienea mitandaoni huku zikimuhusisha kiungo Mshambuliaji wa klabu ya Simba, Mohamed Ibrahim''Mo" kujiunga na klabu ya Yanga.

Hii inaonekana kuwa wazi kwani tayari baadhi ya wanachama wakubwa na klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Jangwani kuanza kuonyesha dalili za makubaliano baina yao na mchezaji huyo.

Mmoja wa wanachama hao ni mtoto wa aliykuwa Raisi wa Tanzania katika awamu ya nne, Mh Riziwani Kikwete amepisti kupitia ukurasa wake wa Instagram picha ya kiungo huyo huku baadhi ya maoni ya wasomaji wa posti hiyo wakionyesha wazi kuwa tayari wameelewa kinachomaanishwa katika picha hiyo.


Hii imetokea ikiwa ni Siku chache baada ya kuelezwa kuwa kiungo huyo hana uhusiano mzuri na kocha wake mkuu, Pierre Lechantre kuna taarifa zimeanza kushika kasi juu ya majaaliwa ya mchezaji huyo.

Mo amekuwa hapati namba katika kikosi cha kwanza licha ya kuwa msimu uliopita alionyesha uwezo mzuri na kutabiriwa na wadau wengi kuwa anaweza kuwa tishio katika kikosi hicho siku za usoni.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.