Samata Awashukuru TFF Baada Ya Tanzania Kupata Ushindi wa 2-0
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipa kunako klabu ya soka ya KRC Genk ya Ubeligiji, Mbwana Ally Samatta amelishukuru shirikisho la soka nchini (TFF) kwa kuandaa mechi ngumu za kirafiki za Kimataifa kwa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars).
Samatta ambaye ndiye nahodha wa kikosi cha Taifa Stars amesema wamepata kujifunza vitu vingi kwa kucheza michezo miwili ya kirafiki na timu ambazo zipo mbali katika ramani ya soka barani Afrika.
“Ni michezo ambayo kama Tanzania tunazihitaji, ni game ngumu lakini mwisho wa siku ukipata matokeo unakuwa umejisogeza kwenye viwango vile vya FIFA lakini pia ukifungwa inakusaidia kukujengea kujiamini na uzoefu zaidi, kwa hiyo ni game ambazo tunazihitaji, kwani mnapokuwa mnakutana kwenye mashindano mnakuwa mnajiamini,” Samatta amesema.
Professional soka
Kadhalika Samatta amewashauri wachezaji wenzake kujitahidi kutoka nje ya Tanzania na kwenda kujaribu soka la huko ili kuweza kujipa uzoefu wa soka la kisasa na baadae kuja kuisaida Tanzania katika mechi kama hizi.
“Wachezaji wote ni wazuri na wanavipaji, lakini kuna kitu unakipata unapokuwa kwenye professional, kwa hiyo tunahitaji tupate wengi zaidi, wachezaji waliopo nyumbani watoke tuijenge timu yetu ya Taifa, njia rahisi ya kuifanya timu yetu iwe na mafanikio ya muda mfupi ni kuwa na wachezaji wengi katika soka la Kimataifa wakati tunasubiri wadogo zetu wakikua,” Samatta ameeleza.
Mechi walizocheza
Nahodha huyo wa Tanzania ameisaidia Taifa Stars kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu ya DR Congo katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo Samatta alifanikiwa kufunga bao la kwanza lakini pia kutengeneza bao la pili ambalo lilifungwa na Shiza Kichuya katika dakika ya 87.
Aidha katika mchezo wa kwanza wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika nchini Algeria Tanzania walichapwa kwa mabao 4-1 na timu ya Taifa ya Algeria, bao pekee la Tanzania katika mchezo huo lilifungwa na Simon Msuva.
Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.