NIYONZIMA SASA ARUDI KIKOSINI, AANZA MAZOEZI.


Kiungo wa Simba, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima, rasmi anaendelea na mazoezi binafsi kwa kujifua ufukweni baada ya kuwa nje kwa muda mrefu kutokana na kuwa majeruhi.

Niyonzima amekuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi mitatu na alikwenda kuti­biwa nchini India Februari, mwaka huu na kutokana na kusumbuliwa na tatizo la enka.

Kutokana na majeraha hayo, kiungo huyo alishindwa kwenda Misri ambapo wenzake walikwenda kucheza mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry.

Niyonzima asema"

“Nashukuru Mungu kwa sasa ninaendelea vyema ndiyo maana nimeanza kufanya mazoezi ili kuanza kujiweka sawa baada ya kupata matibabu na kuanza kure­jea katika hali yangu.

“Nafikiri muda si mrefu nitaunga­na na wenzangu maz­oezini na naamini kuwa baada ya muda nitavaa tena jezi ya Simba,” al­isema Niyonzima.


Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.