Ninje: Kama waCongo wanamiili mikubwa wakanyanyue vyuma


Kocha mkuu wa kikosi cha timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 (Ngorongoro Heroes) Ammy Conrad Ninje amesema njia pekee ya kuwamaliza mapema vijana wa DR Congo ambao wana miili mikubwa ni kucheza kwa kasi na kusukuma mashambulizi muda wote.

Ninje amesema japo hawafahamu kabisa wapinzani wake hao katika mchezo wao wa kufuzu kwenye fainali za Mataifa Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Niger, lakini miili yao inaonesha wazi ni soka gani ambalo wakilitumia basi watawafunga mabao mengi na kujihakikishia kufuzu hatua inayofuata.

“Kama ni wakubwa wakafanye bold building, lakini kwenye football is about pressing, ni kuhusu ufundi na ni kuhusu approach yako ya mchezo, ukiangalia hata timu yetu ya wakubwa ilivyocheza na wao ukiangalia wachezaji wao wengi ni wakubwa, ukiangalia Samatta ana Speed, Msuva pia na mimi nina wachezaji wenye speed nitawatumia,” Ninje amesema.

Kadhalika Ninje amesema kuhusu maandalizi tayari wameshamalizi na wamefanya mazoezi ya mwisho asubuhi, na kwamba wachezaji wana hamu ya ushindi kuliko wakati mwingine wowote, hivyo amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kuja kuwashangilia.

Tutamaliza kazi nyumbani

Kwa upande wake nahodha wa Ngorongoro Heroes Dickson Job amesema wanataka kushinda mabao mengi katika mchezo wa hapa nyumbani ili wakienda Kinshasa wao tayari wamemaliza kila kitu.

“Tumejiandaa vizuri mpaka katika mazoezi ya mwisho, tuko vizuri, wachezaji tuna morali ya hali ya juu, tunachowaomba watanzania wajitokeze kwa wingi kwani tunaimani mechi itakuwa nzuri, lengo letu tunataka mechi tuimalizie hapa hapa nyumbani ili tukiwa tunaenda kwao tuwe tumeshamaliza kila kitu,” Job amesema.

Kama Ngorongoro Heroes watafanikiwa kuwaondoa DR Congo katika hatua hiyo ya raundi ya kwanza watakutana na vijana wa Mali katika hatua ya pili ya kuwania kufuzu kwenye fainali ambazo zitafanyika mwakani nchini Niger.


Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.