Stand United Watangulia Nusu Fainali (ASFC).
Timu ya soka ya Stand United imekuwa timu ya kwanza kukata tiketi ya kucheza nusu fainali ya michuano ya Azam Sports Federations Cup baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi kiduchu wa bao 1-0 dhidi ya timu ya soka ya Njombe Mji.
Wakicheza katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga, Stand United walijipatia bao lao kupitia kwa mshambuliaji Bigirimana Badibakule Blaise baada ya kupokea pasi kutoka kwa Vitalis Mayanga katika dakika ya 12 ya mchezo huo.
Licha ya kufungwa bao hilo Njombe Mji ambao wameshusha kikosi ambacho hakina wachezaji wengi wazoefu walioweza kulichachafya lango la Stand United hasa katika dakika za mwisho za kipindi cha kwanza.
Ni Azam au Mtibwa?
Stand United wanasubiri mshindi kati ya Azam FC na Mtibwa Sugar kucheza naye nusu fainali ambapo mchezo kati ya timu hizo utafanyika leo katika uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi nje kidogo ya jijini la Dar es Salaam.
Mechi nyingine za robo fainali zitakuwa baina ya Tanzania Prisons na JKT Tanzania itakayofanyika leo katika uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, na Singida United dhidi ya Dar Young Africans utafanyika kesho April Mosi katika uwanja wa Namfua mjini Singida.
Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.