Anza Siku Ya Leo Kwa Kuifahamu Habari Hii Kutoka Simba Sc..
Kikosi cha Simba kinaondoka jijini Dar es Salaam leo kuelekea Iringa kuweka kambi ya muda mfupi kabla ya safari ya kuelekea Njombe.
Simba itakuwa Iringa kwa muda mfupi kuendeleza maandalizi ya mechi ijayo katika ligi dhidi ya Njombe Mji FC itakayopigwa Aprili 3 2018.
Kuelekea mchezo huo, Simba inaweza kumkosa kiungo wake, Jonas Mkude aliyeumia kifundo cha mguu wakati kikosi hicho kikifanya mazoezi Uwanja wa Boko Veterani.
Wekundu hao wa Msimbazi, wataondoka Iringa siku moja kabla ya mechi dhidi ya Njombe Mji kuelekea mjini humo tayari kwa mchezo huo.
Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.