Mohamed Ibrahim "MO" Atimuliwa Simba.
Kocha mkuu wa klabu ya Simba, Lechantre amemtimua kiungo, Mohamed Ibrahim 'MO' kikosini mwake baada ya mchezaji huyo kuonyesha vitendo vya utovu wa nidhamu ikiwamo kususia mazoezi.
Habari kutoka Simba zinasema Mfaransa huyo amekuwa akifuatilia kwa karibu tabia za wachezaji wake pasipo wao kufahamu na kiungo huyo amekuwa mhanga wa kwanza kupewa adhabu kali.
"Mohammed Ibrahim ni mchezaji mwenye kipaji, ila tatizo hajitumi. Alipoona hapati nafasi kikosini aliacha kuja mazoezini jambo ambalo lilimkwaza kocha mkuu na kufikia uamuzi huo,” kilisema chanzo chetu.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.