Kikosi Cha Wachezaji 23 wa Congo DR watakoivaa Taifa Stars Machi 27, Dar es salaam


Kocha Mkuu wa timu ya Taifa DR Congo (The Leopards), Florent Ibenge ametangaza kikosi cha wachezaji 23 watakotua Tanzania Jumapili, Machi 25 kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Taifa Stars uwanja wa Taifa Machi 27 jijini Dar es salaam.

Katika kikosi hicho Ibenge amewaita wachezaji sita tu wanaocheza soka nchini Congo, huku wachezaji wengine 17 wkaiwa wanatoka katika vilabu vikubwa barani Ulaya na Asia.

Mchezaji ghali kuliko wote Afrika kwa sasa Cedric Bukambu anayecheza soka nchini China ni miongoni mwa wachezaji walioitwa sambamba na mchezaji nyota na kipenzi cha mashabiki nchini Uingereza Yannick Bolasie.

Kikosi kamili cha DR Congo ni:

Walinda milango: Parfait Mandanda (Charleroi, France ), Joël Kiassumbua (Lugano, Italy ), Matampi Ley (unattached )

Walinzi: Issama Mpeko (TP Mazembe), Ikoko Jordan (EAG, France), Nsakala Fabrice (Alayanspor, Turkey ), Ngonda Glody (AS Vita club), Masuaku Arthur (West Ham, England ), Chancel Mbemba (Newcastle United, England),  Moke Will ( Konyaspor, Turkey ), Bangala Yannick /AS Vita ), Luyindama Christian (Standard, Belgium ), Mulumbu Youssouf ( Kilmanock, Scotland ), Lema Mabidi /Raja, Morocco )

Viungo: Kebano Neeskens (Fulham, England ), Giannelli Imbula (Toulouse, France), Maghoma Jacques (Birmingham, England ), Kakuta Gael (Amiens, France ),

Washambulaji: Bolasie Yannick ( Everton, England), Kabananga Junior (AL Nassr, Saudi Arabia), Mubele Firmin (Toulouse, France ), Paul-José Mpoku (Standard Liege, Belgium ), Cédric Bakambu (Beijing, China ), Afobe Benik (Wolves, England ), Assombalonga Britt (Middlesbrough, England ), Tshibola Aaron (Kilmanock, Scotland )


Join us on WHATSAPP Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.