Hii Ndio Timu Mpya Anayochezea Thomas Ulimwengu...
Jana Baada ya kutagazwa kwa jina la Mshambuliaji wa Thomas Ulimwengu kwenye kikosi cha Tanzania, Taifa Stars kitakachocheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Algeria na DR Congo watu mbalimbali kwenye mitandano ya Kijamii walihoji uhalali wa kuitwa kwa Ulimwengu huku hana timu?
Pamoja na watu wengi kuhoji uhalali wa kocha mkuu wa timu ya taifa ametumia kigezo gani kumuita Thomas Ulimwengu kwenye timu ya Taifa lakini kwenye Taarifa kwa vyombo vya Habari kutoka TFF iliandika Thomas Ulimwengu ni mchezaji wa timu ya FK Sloboda Tuzla ya Bosnia.
Thomas Ulimwengu mwezi saba mwaka jana alipata majeraha ya goti ambayo yalimpelekea kufanyiwa upasuaji aliofanyiwa mwezi wa nane , baada ya kufanyiwa upasuaji alikaa nje kwa muda. mwezi wa 12 klabu yake AFC Eskilstuna ya Sweden ikashuka daraja tena ndio sababu ambazo zinadaiwa Ulimwengu kuachana na klabu hiyo.
Meneja wa Mshambuliaji huyo wa zamani wa Tp Mazembe, Jamal Kasongo amesema ni kweli Thomas Ulimwengu amepata timu Bosnia na kinachosubiliwa ni ITC na vibali vya kufanya kazi katika nchi hiyo.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.