Hii Hapa Ratiba Kamili Ya Robo Fainali Azam Sports Federation.
Hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho 'Azam Sports Federation Cup' inatarajia kuanza kutimua vumbi Ijumaa ya Machi 30 2018 kwa mchezo mmoja kupigwa.
Stand United itakuwa mwenyeji wa Njombe Mji katika Uwanja wake wa nyumbani, CCM Kambarage, mchezo utakaoanza saa 10 kamili jioni.
Baada ya mchezo huo siku ya Ijumaa, ratiba itaendelea tena Jumamosi ya Machi 31 2018 kwa mechi mbili ambapo Tanzania Prisons itaikaribisha JKT Tanzania kwenye Uwanja wa Sokoine Mjini Mbeya huku mechi ikitarajiwa kuanza saa 8 kamili mchana.
Siku hiyohiyo Azam FC itacheza na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Azam Complex, mchezo utaanza saa 2 kamili za usiku.
Hatua hiyo ya robo fainali itakamilika Jumapili, April 1 2018 kwa mchezo mmoja kuchezwa Uwanja wa Namfua kati ya wenyeji Singida United watakaokuwa nyumbani dhidi ya Yanga.
Join us on WHATSAPP
Usipitwe Na Breaking News Za Soka: Jiunge nasi kupitia Facebook, Bofya LIKE Button...
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.