Amka Na Taarifa Hizi Katika Soka Tanzania Leo


Uongozi wa klabu ya soka ya simba umesema haupo tayari kuona wachezaji wake muhimu wakiondoka katika klabu hiyo msimu ujao huku viongozi hao wamesema tayari washaongea na mchezaji huyo na  mchezaji huyo ameahidi kubadilika .


Masau bwire alia na baridi ya Njombe asema hakika  baridi la Njombe si ya kitoto Kuelekea mchezo wao wa leo mchana saa nane afisa habari huyo amesema kuwa timu yake ipo katika hali nzuri kuelekea Mchezo huo Masau bwire amesema kuwa kauli mbiu yao ni ileile ni  kupapasa tu .


Solanus mhagama kuelekea mchezo wa leo dhidi ya Ruvu shooting amesema kuwa kila kitu kipo sawa  kwa upande wao Njombe mji  solanus amesema kuwa wataingia uwanjani  kupambana  kusaka point 3 kwani wasipo shinda mchezo huo hali itakua mbaya kwao alisema solanus mhagama .


Huko Mbeya leo nyasi kuwaka moto Tz Prisons Vitani leo kupambana na wabishi kutoka mwanza Mbao fc kueleka mchezo huo kila upande umejinasibu kutoka na ushindi katika mchezo huo Mchezo huo utapigwa majira ya Jioni huko jijini mbeya .



Maji maji wasema wamekwenda kagera sugar kutafuta point 3 huku uongozi wa timu hiyo ukisema kuwa kila kitu kipo sawa kuelekea mchezo wa  leo .
                  Kwa upande wa kagera sugar wamesema kuwa wataingia  uwanjani kusaka point tatu muhimu mchezo huu  utakao pigwa saa kumi kamili jioni .



Mnyama Simba apunguzwa kasi Uwanja wa taifa  hii ni baada ya kutoka  sare ya goli tatu kwa tatu  dhidi ya  wabishi kutoka Shinyanga Stend United  baada ya matokeo haya kocha wa Simba amesema kuwa wanashukuru kupata point moja na wameyakubali matokeo huku akili yao wakiihamishia katika michuano ya kimataifa .



Nahodha wa Stend united amesema kuwa kwa upande wao wanashukuru kupata point moja kwani ligi kuu msimu huu inaushindani sana  stend wapo nafasi ya nane wakiwa na point 23 .


Azam fc tupo tayari kwa ajili ya kupambana na Singida united kila kitu kipo sawa kuelekea mchezo huo   mchezo huo utapigwa majira ya saa moja usiku katika dimba la Azam complex .



Singida united Azam fc tunakuja kuchukua point tatu katika dimba lenu la chamazi Singida united wamesema kila kitu kipo sawa kuelekea mchezo huo wataingia uwanjani kupambana kupata point 3 muhimu kwani bado wanawinda nafasi za juu za msimamo wa ligi kuu Tanzania bara .



Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara klabu ya soka ya Yanga sc jana wameendelea na Mazoezi kujiandaa na Mchezo dhidi ya town ship rollers ya bostwana mchezo huo  utapigwa jumanne hii katika uwanja wa taifa .



Msanii nasibu Abdul kutumbuiza katika ufunguzi wa kombe ka dunia mwezi wa sita pamoja na mastaa kibao duniani  hongera sana Chibu nenda kaitangaze Tanzania ya wapenda soka .

Yanga sc kupitia Ukurasa wake wa Istagram imeripoti Taarifa hii njema kwa wapenda soka nchini , kwa yeyote atakaye hitaji kwenda na Mabingwa hao mjini Bostwana kwa ajili ya mchezo wa marudiano  dhidi ya Township Rollers mkwanja wake ni USD 498  kwenda na kurudi .


Tff imeripoti kuwa  Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars inatarajia kucheza mechi mbili za kirafiki na Algeria Machi 22,2018 nchini Algeria na DR Congo Machi 27,2018 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam,Tanzania,michezo itakayochezwa kwenye tarehe za kalenda ya FIFA.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.