Simba Kurejea Leo...
Kikosi cha Simba kinatarajia kurejea leo nchini baada ya kucheza mchezo wa marudiano jana dhidi ya Gendarmarie Nationale FC, kikosi cha Simba kinarejea leo baada ya ushindi wa goli moja kwa bila, goli ambalo lilifungwa na mshambuliaji Emmanuel Okwi kunako dakika ya 55 katika kipindi cha pili.
Kwa matokeo hayo sasa kikosi cha Simba kitakutana na timu ya Al Masry SC kutoka nchini Misri, mchezo huu unatarajiwa kuwa kati ya tarehe 9/10/11.
Kikosi cha Simba leo kimefanya mazoezi ya mwisho kabla ya kuanza kujiandaa kurejea nchini kwa kutumia usafiri wa ndege kupitia KQ saa 12:05.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.