Habari Kubwa katika Soka Tanzania Leo Jumatano.
Emanuel Okwi Baada ya kuumia katika mchezo wa Juzi jumatatu dhidi ya Mbao fc uongozi wa klabu ya soka ya Simba umesema kuwa Emanuel okwi anaendelea vyema huku Daktari wa timu ya Simba Dk Yasin Gembe akisema nyota huyo atakuepo katika kikosi kitakacho cheza na stend ijumaa hii .
Bodi ya ligi imeurudisha nyuma mchezo wa Simba Vs Stend sasa kuchezwa ijumaa hii huku sababu kubwa ikiwa ni simba kutaka kufanya maandalizi mapema kuhusu mchezo wao kombe la shirikisho dhdi ya Alamsry .
Kuelekea mchezo wa Simba dhidi ya Stend united kikosi cha stend united kimeendelea na maandalizi ya mchezo huo utakao pigwa jijini Dar es laam ijumaa hii.
Kikosi cha wanalizombe Maji Maji fc kimeondoka leo mjini Songea kuwafata wakatamiwa wa mkoani bukoba kagera sugar .
Kutoka bodi ya ligi imetangaza kuwa mchezo kati ya Lipuli fc dhidi ya ndanda umesogezwa mbele sasa utachezwa march Nne baada ya march 2.
Kocha mkuu wa mvuvumwa Joseph kanakamfumu amefungiwa na shirikisho la soka nchini kwa muda wa miaka mitano kutojihusisha na masuala ya soka huku chanzo kikiwa ni kugushi usajili wa wachezaji walio sajiliwa katika klabu yao .
Kuelekea mchezo wa Yanga dhidi ya ndanda uongozi wa klabu ya soka ya Yanga umesema kuwa kila kitu kimekamilka kuelekea mchezo huo huku uongozi huo ukiwaomba wanaYanga mkoani mtwara kuja kuwapa Sapoti.
Kwa upande wa Uongozi Ndanda wao wamewaomba wanamtwara kujitokeza kwa wingi kuja kuwapa hamasa wachezaji wao katika mchezo huo unangojwa kwa hamu na wapenzi wa soka nchini .
Klabu ya Mbeya city hakuna kulala ni mwendo wa Mazoezi sasa akili yao yote ipo kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania dhidi ya mwadui fc watakao kutana nao wiki hii.
Kufuzu Afcon ya wanamama Timu ya Taifa ya wanawake nchini Tanzania twiga stars kucheza na Zambia jijini Dar es laam bado tarehe haijapangwa kwa mujibu wa Afisa habari msaidizi wa Tff.
Yanga kuchezeshwa na waburundi katika Ligi ya Mabingwa Barani Africa dhidi Township Rollers
1 Mwamuzi wa kati atakuwa Pacifique Ndabihawenimana
2 Mwamuzi msaidizi namba moja Willy Habimana
3 Mwamuzi msaidizi namba mbili Pascal Ndimunzigo
3 Kamishna wa mchezo huo anatoka Swaziland Mangaluso Jabulani
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.