Manara Awasifia KMKM Atoa Taarifa Hii Kwa Vyombo Vya Habari.



Mara baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya KMKM dhidi ya Simba sc na Simba kuibuka na ushindi wa goli 1-0, afisa habari wa timu hiyo , Haji Manara amewapongeza KMKM kwa kiwango kizuri walichokionuesha kwenye mchezo huo.

Aidha Manara ameongeza kwa kuweka wazi kua kesho majira ya saa sita mchana atakuwa na mkutano na wanahabari kuzungumzia kuelekea mchezo wa klabu bingwa Afrika dhidi ya klabu ya Js Saoura utakaopigwa jumamosi kunako uwanja wa taifa.

"Mazoezi mazuri tumeyapata  toka kwa KMKM na burudani ya kutosha wamepata Wazanzibar toka kwetu
Thanks God
Nb
kesho Jumatatu Saa sita kamili mchana ya tarehe 7/1/2019 ntaongea na Wanahabari kuelezea maandalizi ya Mchezo mkubwa dhidi ya Waalgeria jumamosi ,Mkutano huo utafanyika Makao Makuu ya klabu Mtaa wa Msimbazi hapa jijini Dar es Salaam ,Inshaallah 🙏"

Ikumbukwe kuwa timu hizo zipo kundi D pamoja na klabu za Al Ahly na As Vita club ya Congo.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.