Waamuzi TPL wapigwa stop kwa kupuyanga
Kamati ya Waamuzi ya shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia kwa mwenyekiti wake Mzee Salum Chama imewasimamisha baadhi ya waamuzi ambao wameboronga kwenye michezo ya raundi ya kwanza na ya pili ya ligi kuu Tanzania Bara (TPL)
-Waamuzi waliosimamishwa kupisha uchunguzi mwamuzi msaidizi namba 2 (Line 2) Godfrey Msakila kutoka Geita mchezo kati ya Yanga SC dhidi Mtibwa Sugar, Msakila anadaiwa kukataa goli la Makambo kwa kudai mfungaji alikuwa kwenye eneo la kuotea.
-Mwamuzi mwingine ni Sylvester Mwanga kutoka Kilimanjaro (Line 2) mchezo wa Yanga dhidi ya Mtibwa naye amesimamishwa kwa kulalamikiwa kuzuia shambulizi la Mtibwa akidai Ismail Aidan alikuwa ameotea huku picha za video za marudio ya tukio hilo zikionyesha hakuotea.
-Pia refa wa kati Nassoro Mwinchui na msaidizi wake Abdallah Rashid wa Pwani wamesimamishwa kwa kosa la kukataa goli la Biashara United katika mechi ya Coastal Union dhidi ya Biashara wakidai mfungaji alikuwa ameotea.
-Wengine ni Mwamuzi msaidizi Nicholas Makaranga wa Morogoro amesimamishwa kwa kukataa goli la Ruvu Shooting dhidi ya KMC akidai mfungaji Fully Zullu Maganga alikuwa kwenye nafasi ya kuotea.
-Pia Rungu hilo la kusimamiahwa limemkuta msaidizi Ahmada Jamada kutoka Kagera ambaye alikataa goli la kusawazisha la Mwadui FC dhidi ya Singida United juzi Jumapili kwa madai ya kuwa mfungaji alikuwa ameotea
-Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mzee Salum Chama alisema waamuzi hao walichezesha chini ya kiwango na kupata Alama chache zilizopelekewa kusimamishwa kupisha uchunguzi kabla ya kuchukuliwa hatua zaidi.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.