Sio tu Afrika Mashariki bali hata Kusini pia Simba Sc ndio baba lao Instagram.


“This is Simba” hiyo ni sauti ya Haji Manara msemaji wa Simba ambayo asubuhi ya leo ilinilazimisha kujaribu kuangalia upande wa pili wa ukubwa wa Simba Sc mtandaoni.



Nikagundua hakuna klabu katika Afrika Mashariki wala Afrika ya Kusini ambayo inaikuta klabu ya Simba kwa followers wengi katika mtandao wa Instagram.



Katika mtandao huo Simba wana jumla ya wafuasi 321k(321,000+) hii ikiwa idadi kubwa zaidi ya watani wao Yanga walioko nafasi ya pili wakiwa na jumla ya wafuasi 163k(163,000).



Azam Fc wako nafasi ya tatu kwa hapa Tanzania wakiwa na followers 129k(129,000), na kisha wanafuatia Mbeya City ya mjini Mbeya ambao wao wana jumla ya followers 74k(74,000)



Singida United wenyewe wanakuja baada ya Mbeya City wakiwa na followers 70.5k(70,000), na baada ya hao kuna Mtibwa Sugar wanafuatia wakiwa na jumla ya followers 68.6k(68,600+).



Kwa ligi kuu ya nchini Kenya hakuna timu ambayo inawashika Wekundu wa Msimbazi kwani kinafa wa huko katika Instagram ni Gormahia Fc ambao wana wafuasi 22k tu katika Instagram.



Klabu za Afrika Kusini nazo hakuna anayemgusa Mnyama, bali anayemkaribia Simba ni Keizer Chief ambao wenyewe wana followers 318k, Orlando Pirates wana 70.6k, Mamelody Sundowns 93.8k.

Source: Shaffihdauda

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.