Samatta azidi kuwika Ubelgiji aipa ushindi timu yake tena akitokea benchi.

-Mshambuliaji wa Tanzania Mbwana Samatta jana alifanikiwa kuisaidia klabu yake ya Genk kushinda mchezo wa ligi kuu Ubelgiji kwa magoli 3-2 dhidi ya Waasland Beveren baada ya kutokea Bechi dakika 59 wakiwa nyuma kwa magoli mawili kwa moja (2-1)

-Samatta aliingia kuchukua nafasi ya Zinho Gano dakika ya 59 na kufanikiwa kuisawazishia timu yake dakika 78 kabla ya Caufriez kujifunga goli dakika ya 89. Kwa sasa Genk wanaongoza msimamo wa ligi kuu Ubelgiji (First Division) wakiwa na pointi 13 baada ya kucheza mechi 5 na kushinda mechi 4 na kutoa sare mchezo mmoja sawa na Club Brugge wenye pointi 13.

-Samatta msimu huu amefanikiwa kufunga magoli 8 katika mechi 10 alizocheza ikiwa mechi 5 za Uefa Europa League na mechi 5 za ligi kuu ya Ubelgiji kati ya magoli 8 magoli 5 amefunga katika Uefa Europa League na 3 katika ligi kuu ya Ubelgiji.

-Genk ya Samatta itachuka uwanjani tena August 30 kucheza na Brøndby katika uefa Europa League na September 02 watacheza mchezo wa ligi kuu na Kortrijk baada ya hapo Mbwana Samatta atajiunga na timu ya Taifa kwa ajili ya mchezo wa kufuzu Afcon 2019 dhidi ya Uganda

FT KRC Genk 3-2 Waasland Beveren
  20' Zeghrova      66' Ampomah
  78' Samatta        75' Ampomah
  89' Caufriez (og)

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.