Matumaini ya Yanga ya kushinda Mchezo dhidi ya Rayon Sports na taarifa ya majeruhi wa Yanga.


Uongozi wa klabu ya Yanga umesema maandalizi baina yao na Rayon Sports kuelekea mechi ya Ko..mbe la Shirikisho Afrika leo yanaendelea vizuri huko Kigali, Rwanda.

Mratibu wa timu, Hafidh Saleh, amesema wachezaji wote wako vizuri kiafya na hakuna yoyote ambaye yuko majeruhi.

Saleh ameeleza lengo lao kubwa kwenye kipute hicho ni kuweka heshima ya kuhakikisha wanapata matokeo licha ya kuwa hawana nafasi ya kusonga mbele.

Yanga itashuka dimbani kucheza mchezo wa kukamilisha ratiba na Rayon kutokana na kutokuwa na nafasi tena ya kusonga mbele

Mechi hiyo itaanza majira ya saa 10 kamili kwa saa za Afrika Mashariki ambapo itachezwa kwenye Uwanja wa Nyamirambo uliopo jijini Kigali

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.