Wachezaji Hawa Ndio Wenye Ruhusa Ya Kucheza Michuano Ya SportPesa Super Cup.


Wachezaji wenye mikataba kamili wataruhusiwa kucheza michuano ya SportPesa Super Cup inayoanza keshokutwa Juni 03 Nakuru Kenya hata kama wamesajiliwa wakati huu, imefahamika.

Ufafanuzi huo umetolewa kufuatia sintofahamu iliyojitokeza baada ya tangazo la awali kubainisha kuwa wachezaji wapya waliosajiliwa na timu za Tanzania wakati huu hawaruhusiwi kushiriki michuano hiyo.

Sasa watakaoweza kucheza ni wale ambao tayari wamemaliza mikataba yao ya kuzitumikia timu zao za zamani na tayari wamesaini mikataba kamili katika timu zinazoshiriki michuano hiyo.

Wachezaji waliosaini mikataba ya awali hawataruhusiwa kushiriki michuano hiyo.

Hii ina maana kwamba kwa wale wachezaji waliosajiliwa lakini mikataba yao inamalizika mwishoni mwa mwezi huu au mwezi ujao hawataruhusiwa kushiriki michuano hiyo.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.