Taarifa Kutoka Azam Kuhusu Jeraha La Ngoma


Daktari wa timu ya Azam, Mwanandi Mwankemwa amethibitisha kuwa mshambuliaji Donald Ngoma atakuwa nje ya uwanja kwa wiki tisa.

Dokta Mwankemwa amerejea leo saa tatu asubuhi kutoka Afrika Kusini alipokwenda kufanyiwa vipimo katika hospitali ya St. Vincent Parrot.

Mwankemwa amesema Ngoma alikuwa ana uvimbe kwenye goti la kulia ambapo baada ya vipimo imeonekana alikuwa amechanika kidogo japo tayari ameanza kupona.

Hata hivyo dokta huyo aliongeza kuwa Ngoma hatafanyiwa upasuaji badala yake ataendelea kufanya mazoezi mepesi ya kawaida mwenyewe kabla ya kupona kabisa na kurejea uwanjani.

"Vipimo alivyofanyiwa Ngoma vinaonyesha atakaa nje ya uwanja kwa wiki tisa ili kupona kabisa ambapo itakuwa hadi mwezi wa Agosti," alisema Dk. Mwankemwa

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.