Kauli Ya Kocha Masoud Djuma Kuelekea Mchezo Wa Kesho

Kaimu kocha mkuu wa timu ya Simba, Masoud Djuma amesema katika mchezo wa kesho wa fainali dhidi ya Gor Mahia watacheza tofauti na watu walivyozoea.

Katika michezo miwili iliyopita dhidi ya Kariobangi Sharks na Kakamega Homeboyz, Simba haikuwa kwenye kiwango bora sana kitu ambacho kocha Masoud ameahidi kutotokea kesho.

Masoud amesema ingawa hawapewi nafasi kubwa ya kufanya vizuri kuliko wapinzani wao Gor lakini wamejipanga kufanya maajabu na kurejea na kombe nyumbani.

Raia huyo wa Burundi ameongeza kuwa siku zote mchezo wa fainali unakuwa wa tofauti na amewaandaa wachezaji wake vizuri na watu wategemee mchezo wa tofauti kesho.

"Kesho tutaingia kivingine kabisa kuliko tulivyocheza mechi zilizopita, wenzetu wefunga mabao matano sisi hatujafunga hata moja lakini kesho tutafanya hivyo.

Mungu ndio anajua nani atachukua ubingwa lakini sisi tutapambana mpaka tone la mwisho," alisema Masoud.

Mchezo huo wa fainali utachezwa katika uwanja wa Afraha kuanzia saa 9 alasiriKaimu kocha mkuu wa timu ya Simba, Masoud Djuma amesema katika mchezo wa kesho wa fainali dhidi ya Gor Mahia watacheza tofauti na watu walivyozoea.

Katika michezo miwili iliyopita dhidi ya Kariobangi Sharks na Kakamega Homeboyz, Simba haikuwa kwenye kiwango bora sana kitu ambacho kocha Masoud ameahidi kutotokea kesho.

Masoud amesema ingawa hawapewi nafasi kubwa ya kufanya vizuri kuliko wapinzani wao Gor lakini wamejipanga kufanya maajabu na kurejea na kombe nyumbani.

Raia huyo wa Burundi ameongeza kuwa siku zote mchezo wa fainali unakuwa wa tofauti na amewaandaa wachezaji wake vizuri na watu wategemee mchezo wa tofauti kesho.

"Kesho tutaingia kivingine kabisa kuliko tulivyocheza mechi zilizopita, wenzetu wefunga mabao matano sisi hatujafunga hata moja lakini kesho tutafanya hivyo.

Mungu ndio anajua nani atachukua ubingwa lakini sisi tutapambana mpaka tone la mwisho," alisema Masoud.

Mchezo huo wa fainali utachezwa katika uwanja wa Afraha kuanzia saa 9 alasiri

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.