VIDEO: Kichuya Agomewa Kusaini Mkataba Mpya Simba, Sababu Hii Hapa.


BABA Mzazi wa Kiungo Mshambuliaji wa Simba Shiza Kichuya mzee Ramadhani Kichuya amemzuia mwanaye kuongeza mkataba mwingine mpya wa kuendelea kuichezea timu hiyo hadi atakapojua muafaka wake wa kwenda klabu ya TP Mazembe ya DR Congo.
Mazembe ni kati ya klabu zilizoonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji huyo ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika juni mwaka huu wakati Ligi Kuu Bara ikiwa imemalizika.

No comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.