Tetesi Zote Za Usajili Ulaya Leo Jumapili..
Manchester United wana mpango wa kumchukua mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar huku klabu hiyo ya Old Trafford ikipambana na Real Madrid kupata sahihi ya mchezaji huyo 26 mwenye asili ya Brazil (Sunday Mirror)
Unai Emery, ambaye ataondoka Paris St-Germain mwishoni mwa msimu, amekuwa gumzo, akipendekezwa kuchukua mikoba ya Arsene Wenger, Meneja wa Arsenal (Sunday Express)
Hata hivyo, West Ham wanamhitaji Emery achukue mikoba ya David Moyes. Meneja wa zamani wa Manchester City Manuel Pellegrini na meneja wa zamani wa Watford Marco Silva wanamtamani Emery.(Sun on Sunday)
Meneja wa Juventus Massimiliano Allegri, anataka kitita cha pauni milioni 200 kama atakuwa meneja wa Arsenal.(Sun on Sunday)
Manchester City inataka saini ya kiungo wa kati wa Napoli,Jorginho, 26, na mshambuliaji wa pembeni Riyad Mahrez, 27, wa Leicester kwa gharama ya takriban pauni milioni 110 (Mail on Sunday)
Juventus inataka kumsajili tena mshambuliaji wa Chelsea Alvaro Morata 25, kipindi cha majira ya joto huku mshambuliaji Mario Mandzukic akijiandaa kuiacha klabu hiyo. (Sky Sports)
Liverpool italipa pauni milioni 52.75 kwa kiungo wa kati Naby Keita 23, baada ya timu yake RB Leipzig kufuzu ligi ya Europa.(Liverpool Echo)
Juventus inajiandaa kupata saini ya kiungo wa kati wa Liverpool Emre Can,24, baada ya fainali ya ligi ya mabingwa (Talksport)
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.