SportPesa Yazicharukia Simba Na Yanga, Zaionya Jambo Hili.
Ule mpango wa vilabu vya Simba na Yanga kuwatumia wachezaji wake wapya kwenye michuano ya SportPesa Super Cup inayoanza Nairobi Juni 03 umekwama baada ya waandaaji wa michuano hiyo kukataa.
Kampuni ya SportPesa inayoandaa mashindano hayo yanayohusisha timu ambazo zinadhaminiwa na kampuni hiyo, imezitaka timu shiriki kutoka Tanzania kutumia vikosi vyao vilivyomaliza msimu.
Huenda timu zikalazimika kuongeza wachezaji wa vikosi vyao vya pili kuziba mapengo ya wachezaji ambao watakuwa wameondoka baada ya kumaliza mikataba.
Yanga ilitangaza kutumia mashindano hayo kutambulisha wachezaji wake wapya na wengine inaokusudia kuwasajiliwa.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.