SINGIDA YAMUUZA RASMI KUTINYU MIL. 45 KWENDA KLABU HII VPL
SINGIDA United rasmi imemuuza kiungo wake mshambuliaji raia wa Zimbabwe, Tafadzwa Kutinyu dola 20, 0000 (sawa na shilingi milioni 45) kwenda Azam FC iliyokuwa inamuwania.
Hiyo ikiwa ni siku chache kuwepo na taarifa za kiungo huyo kuwaniwa na Simba ambayo ilikuwa inamuwinda vikali kwa ajili ya kukiimarisha kikosi chao.
Kutinyu ni mchezaji wa pili kutua Azam baada ya hivi karibuni kufanikisha usajili wa mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo Championi Jumatano inazo, kiungo huyo anatua kuichezea Azam akisaini mkataba wa miaka miwili.
“Kutinyu rasmi ni mchezaji wa Azam, hiyo ni baada ya kufikia makubaliano mazuri kati ya Singida na Azam yenyewe ambayo imekubali kununua mkataba wake wa mwaka mmoja alioubakisha.
“Ni kiasi cha dola 20,000 ambacho kimetosha Singida kumuachia kiungo huyo na kusaini Azam na usajili huo tunaufanya kwa ajili ya msimu ujao ambao tumepanga kuchukua ubingwa,”alisema mtoa taarifa huyo kutoka Azam.
Alipotafutwa Meneja wa Azam, Philip Alando kuzungumzia hilo, simu yake ya mkononi iliita bila ya mafanikio, lakini hivi karibuni alitamba kufanya usajili mkubwa wa kutikisa ndani ya siku mbili kwa maana ya juzi na jana.
No comments:
Note: only a member of this blog may post a comment.